Ugumu utetezi wa haki za binadamu wabainishwa
Dar/Dodoma. Wakati dunia ikiadhimisha siku ya haki za binadamu, imeelezwa kuwa watetezi wa haki za binadamu wanapitia mazingira magumu kutokana na sheria kandamizi, udhaifu wa mfumo wa haki na udhibitiwa kwa vyombo vya habari. Hayo yameelezwa leo Desemba 10, 2024 katika kongamano la haki za binadamu lililoandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania…