Mafuta yashuka Zanzibar ikikaribisha uwekezaji zaidi

Unguja. Wakati mafuta ya petroli na dizelI yakishuka bei, Serikali imesema itaendelea kuweka mazingira wezeshi kuhakikisha upatikanaji wa huduma hiyo unazidi kuimarika. Lakini pia imesema inawakaribisha wawekezaji zaidi kuwekeza katika nishati hiyo hususani kisiwani Pemba. Bei ya petroli imeshuka kutoka Sh2,882 hadi Sh2,775 ikiwa ni tofauti ya Sh107 sawa na asilimia 3.72, huku dizeli ikishuka…

Read More

Msuva na matarajio Afcon 2025

Mshambuliaji mahiri wa Taifa Stars, Simon Msuva ameendelea kudhihirisha umuhimu wake kwa soka la Tanzania kwa mabao yake muhimu katika safari ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Mabao aliyofunga dhidi ya Ethiopia na Guinea yamechochea mafanikio ya Stars na kumkaribisha kwenye rekodi ya kihistoria ya Mrisho Ngassa, mfungaji bora wa muda wote…

Read More

Tasisi ya Wanawake na Samia Dar waadhimisha miaka 63 ya Uhuru kwa usafi kuona wagonjwa

TAASISI ya Wanawake na Samia Mkoa wa Dar es Salaam, imesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ni miongoni mwa mafanikio makubwa ambayo Tanzania inajivunia inapoadhimisha miaka 63 ya  Uhuru wa Tanganyika. Hayo yalielezwa na Makamu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo,  Hanifa Mrisho, alipoongoza wanachama   wa taasisi hiyo  kufanya usafi na kufariji wagonjwa katika hospitali mbalimbali mkoani…

Read More

Zanzibar Yachukua Nafasi ya Makamu wa Rais wa EALS

Katika hatua muhimu kwa Zanzibar, Masoud Salim ameapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jumuiya ya Wanasheria wa Afrika Mashariki (EALS), chombo kinachoongoza kwa wataalamu wa sheria katika ukanda huu. Salim, wakili mashuhuri visiwani Zanzibar, alichaguliwa wakati wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Jumuiya ya Wanasheria Zanzibar mwezi Oktoba na kuthibitishwa rasmi katika Mkutano Mkuu wa…

Read More

HAKIKISHA UNAJIUNGANISHA KWENYE AMANI NA UZALENDO WA TAIFA LAKO

LNa. Vero Ignatus, Arusha Katika kuadhimiasha Miami 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara Mkuu wa Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana viongozi mbalimbali wa madhebu ya dini,wazee wa Kimila wamefanya maombi maalum kwaajili ya kuliombea Taifa.  Maombi hayo yamefanyika leo jumatatu 9 disemba 2024 Azimio la Arusha ambapo maelfu wamejitokeza kwenye  matembezi  ambayo yalianza majira ya…

Read More

Imani ya Simba imebaki Kwa Mkapa 

Tukutane kwa Mkapa ndicho mashabiki wa Simba wanaweza kusema kutokana na hesabu zilivyo kwa timu yao baada ya kupoteza jana, Jumapili kwa mabao 2-1 huko Algeria dhidi ya CS Constantine kwenye mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika katika hatua ya makundi. Katika mchezo huo ambao ulichezwa kwenye Uwanja wa Mohamed Hamlaoui mjini Constantine,…

Read More

Siri ya Uhuru wa Tanganyika

Wakati Tanzania Bara ikiadhimisha miaka 63 ya Uhuru, ni wazi kuwa uwezo wa kujenga hoja wa Mwalimu Julius Nyerere ulikuwa kiini cha kufanikisha Uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza Desemba 9, 1961. Katika kitabu “Tanganyika’s Independence Struggle” kilichoandikwa na Pius Msekwa, Spika mstaafu wa Bunge la Tanzania na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Msekwa…

Read More