Sh110 bilioni kuboresha mashamba ya misitu, mikoko
Dar es Salaam. Tanzania imesaini mkataba wa Euro 39.9 milioni (sawa na zaidi ya Sh109.83 bilioni) na Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD), kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa mashamba ya miti ya Serikali na kuhifadhi misitu ya mikoko. Mradi huu unalenga kuziba pengo hilo kwa kupanda hekta 22,500 za miti ndani ya miaka mitano…