Mama Asimwe akabidhiwa nyumba na UVCCM Kagera
Muleba. Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera umemkabidhi nyumba yenye thamani ya Sh12 milioni, mama mzazi wa marehemu mtoto mwenye ualbino, Asimwe Novath aliyeuawa na kunyofolewa baadhi ya viungo vyake. UVCCM mkoani humo waliahidi kumjengea nyumba mama huyo, Judith Richard baada ya kukumbwa na tukio la kuuawa kwa mwanaye, Asimwe,…