NENDENI MKALETE MAPINDUZI KWA KUSHUGHULIKIA MREJESHO KATIKA OFISI ZA UMMA-BI. LEILA MAVIKA

Na.Lusungu Helela- Dodoma Mwakilishi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, UTUMISHI, Bi. Leila Mavika amewataka Waratibu wa Kushughulikia Mrejesho wakayatumie mafunzo waliyoyapata kuleta mapinduzi katika Madawati au Ofisi za Mrejesho zilizopo katika Taasisi zao ili kufanikisha ushughulikiaji mrejesho kwa ufanisi na kwa wakati katika Ofisi za Umma kwa vile wameaminiwa kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi….

Read More

Ofisa TRA aliyeshambuliwa Tegeta kwa Ndevu afariki dunia

Dar es Salaam. Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Amani Simbayao ambaye ni miongoni mwa maofisa watatu walioshambuliwa na wananchi Tegeta kwa Ndevu jijini Dar es Salaam wakati akitaka kukamata gari linalodaiwa kuingizwa nchini kimagendo, amefariki dunia. Taarifa za kifo chake zimetolewa leo usiku Ijumaa Desemba 6, 2024 na mamlaka hiyo kupitia taarifa kwa…

Read More

Waliojaribu Kumteka Tarimo Kizimbani, Warudishwa Rumande

Na Karama Kenyunko Michuzi Tv WATUHUMIWA sita wanaodaiwa kufanya jaribio la kumteka Mfabyabiashara Deogratius Tarimo wamepelekwa gerezani baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana dhidi ya kosa lao hilo. Washtakiwa baada ya kusomewa kesi yao, mahakama iliwapa masharti ya dhamana ambapo kila mshtakiwa alipaswa kuwa na wadhamini wawili wenye barua za utambulisho kutoka kwa mwajiri…

Read More

TCAA YAADHIMISHA SIKU YA USAFIRI WA ANGA DUNIANI

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imeadhimisha Siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD) mwaka 2024 kwa kupandisha bendera ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga Duniani(ICAO), katika hafla iliyofanyika Makao Makuu ya Mamlaka hiyo Banana-Ukonga jijini Dar es Salaam. Akizungumza na watumishi, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga…

Read More

Majaliwa aionya tume uchunguzi ajali ya Kariakoo

Arusha. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, amewaonya wajumbe wa tume ya wataalamu ya uchunguzi wa ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa nne Kariakoo jijini Dar es Salaam, kutokulindana na kuwaficha wahusika wa uzembe uliosababisha ajali hiyo. Aidha amesema ripoti ya tume hiyo haitasaidia eneo la Kariakoo peke yake bali itatumika kote nchini kusimamia ujenzi uwe…

Read More

Ukamataji unavyozua hofu ya utekaji

Dar es Salaam. Ukiukaji wa utaratibu wa ukamataji unaofanywa na vyombo vya dola, umezua hofu miongoni mwa wananchi, ambao wanauhusisha na matukio ya utekaji. Katika siku za hivi karibuni kumeibuka matukio ya watu kukamatwa yakihusishwa na utekaji, huku mengine yakihusisha watendaji wa vyombo hivyo. Tukio la hivi karibuni ni la dereva ambaye kwa sasa anashikiliwa…

Read More

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU ILI SEKTA YA BAIASHARA IWE YENYE USHINDANI, VIWANGO VYA KIMATAIFA

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha miundombinu ili sekta ya Biashara iwe na ushindani wenye viwango vya Kitaifa na Kimataifa. Waziri Jafo ameyasema hayo katika Maadhimisho ya kitaifa ya siku ya ushindani Duani yaliyofanyika leo Disemba 5,…

Read More