Wanafunzi wa kike TPC wafaidika na juhudi za kiwanda cha sukari
Na Safina Sarwatt, Kilimanjaro Wanafunzi 68 wa kike katika Shule ya Sekondari ya TPC mkoani Kilimanjaro wamepata afueni kubwa baada ya kiwanda cha sukari cha TPC kukamilisha ujenzi wa bweni jipya. Hatua hii imetatua changamoto ya kutembea umbali wa kilomita 20 kwenda na kurudi shuleni kila siku, hali iliyokuwa ikihatarisha usalama wao na kuathiri masomo….