Baba adaiwa kujinyonga baada ya kumchinja mtoto wake

Shinyanga. Mkazi wa Kijiji cha Mwamagunguli, Kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga mkoani humo, Peter Makoye (45) amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ndani ya nyumba yake. Tukio hilo limetokea leo Jumatatu, Desemba 2, 2024, saa 11 alfajiri, huku marehemu akidaiwa kuchukua uamuzi huo muda mfupi baada ya kudaiwa kumjeruhi mtoto wake wa kike mwenye umri…

Read More

Samia amteua bosi MOI, mwenyekiti bodi ya PSSSF

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Balozi Dk Mpoki Ulisubisya kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI). Taarifa ya uteuzi wa Dk Mpoki imetolewa leo Jumatatu Desemba 2, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Sharifa Nyanga. Vilevile katika taarifa hiyo, Joyce Mapunjo ameteuliwa…

Read More

Mzee akutwa ameuawa Moshi, mwili watelekezwa nyumbani kwake

Moshi. Isaack Mallya (72), mkazi wa Kijiji cha Umbwe Onana, Kata ya Kibosho Magharibi, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro amekutwa ameuawa nyumbani kwake na watu wasiojulikana, huku mwili wake ukiwa ukitelekezwa nje ya nyumba hiyo. Mwili wa Mallaya umekutwa asubuhi ya leo Jumatatu, Desemba 2, 2024 ukiwa na majeraha sehemu mbalimbali. Kamanda wa Polisi Mkoa…

Read More

Bondia aliyefariki Zanzibar kwa kupigwa TKO, azikwa Dar

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Abassi Mselem, ambaye Novemba 30, 2024 alipigwa ulingoni na kupoteza fahamu kisha kufariki Desemba 1, 2024, amezikwa leo jijini Dar es Salaam. Mselemu amezikwa kwenye makaburi ya Saku yaliyopo Mbagala jijini Dar es salaam baada ya mwili wake kuwasili leo asubuhi ukitokea Zanzibar. Mweka Hazina wa Chama cha Makocha…

Read More

Jela kwa kutumia laini ya simu ya mtu mwingine

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu Ernest Lwila (30) kulipa faini ya Sh5 milioni au kutumikia kifungo cha miezi sita gerezani, baada ya kupatikana na hatia kwa kosa la kutumia laini ya simu iliyosajiliwa kwa jina la mtu mwingine. Pia, mahakama hiyo imemuachia huru mshtakiwa huyo katika shtaka la kuchapisha taarifa za…

Read More

Yas yataja sababu kubadili jina, vipaumbele

Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mpito wa Kampuni ya Yas Tanzania, Jerome Albou ametaja sababu zilizoifanya kampuni hiyo kubadili jina kutoka Tigo. Albou amesema lengo lao kuu ni kutaka kuboresha huduma za mtandao ili ziwe za kisasa zaidi huku zikimgusa kila mtu. Ofisa huyo amesema hayo leo Jumatatu Desemba 2, 2024 alipofanya mazungumzo…

Read More