Mahakama Kuu yatupa maombi ya Mdude, aendelea kushikiliwa
Mbeya. Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya imetupilia mbali maombi ya mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mdude Nyagali, aliyekuwa akiomba kufikishwa mahakamani au kuachiwa huru tangu akamatwe na polisi Novemba 22, mwaka huu. Maombi hayo yaliwasilishwa na mawakili wa kujitegemea, Boniface Mwabukusi na Philipo Mwakilima, mbele ya Jaji Mussa Pomo. Shauri hilo lilianza…