Wakazi wa Ngombo walalama Serikali kuwahamisha bila kuwapatia maeneo

Malinyi. Wanakijiji wa Ngombo, wilayani Malinyi mkoani Morogoro wameilalamikia Serikali kwa kuanzisha oparesheni ya kuwaondoa katika kijiji hicho kupisha Pori la Akiba la Kilombero, bila kuwapatia eneo mbadala la kuhamia. Wanakijiji hao, walioko katikati ya Bonde la Kilombero, wamekubali kuondoka lakini wanahoji; wataenda wapi? Mkazi wa kijiji hicho, David Mkumba amesema alizaliwa Ngombo, na wazazi…

Read More

Taifa Stars uhakika Afcon, Guinea yaangukia pua CAF

Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) imetupilia mbali rufaa ya Guinea dhidi ya Tanzania na hivyo kuipa uhakika Taifa Stars kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon 2025) nchini Morocco. Guinea ilikata rufaa hiyo baada ya mchezo namba 143 wa kuwania kufuzu Afcon baina yao na Tanzania uliochezwa katika Uwanja…

Read More

Auawa akidaiwa kuchomwa kisu, amani yatawala Krismasi

Dar/ Mikoani. Wakati Watanzania wakiungana na Wakristo duniani kote kuadhimisha Sikukuu ya Krismasi hali ya amani imetawala nchini jana, huku tukio la mauaji ya mfugaji na mkazi wa Lubungo wa Mvomero mkoani Morogoro, Elisha Lengai (20) likitia doa. Lengai anadaiwa kuchomwa kisu na Sikonye Kipondo (22) baada ya kutokea ugomvi ambao chanzo chake bado hakijafahamika….

Read More

Desemba ya ajali, wengine 20 wafa Rombo, Tanga

Handeni. Unaweza kusema Desemba hii ni ya majonzi na simanzi kubwa kutokana na mfululizo wa ajali mbaya zilizotokea, zikiwamo zilizotokea jana wilayani Handeni Mkoa wa Tanga na nyingine iliyotokea leo Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro ambazo zimesababisha vifo vya watu 20. Mwezi huu ambao kwa kawaida huwa wa shamrashamra za sikukuu za mwisho wa mwaka,…

Read More

Utata mauaji ya mtoto wa mfanyabiashara maarufu Dom, azikwa

Dodoma. Utata umegubika tukio la mauaji ya Graison Kenyenye (6), mtoto wa mfanyabiashara maarufu wa jijini Dodoma, Zainab Shaban maarufu  Jojo. Graison aliuawa usiku wa kuamkia juzi, wakati mama yake alipokwenda matembezini na rafiki yake wa kiume. Tukio hilo lilitokea Ilazo Extension jijini Dodoma, usiku wa kuamkia Desemba 25, 2024, wakati Jojo alipomuacha mtoto huyo…

Read More

MAPACHA WAHITAJI MSAADA BAADA YA MAMA YAO KUPATA MARADHI YA MOYO ALIPOJIFUNGUA

Baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Kongowe Kibaha mkoani Pwani wakiwajulia hali watoto mapacha ambao mama yao amepata maradhi ya moyo baada ya kujifungua. ……………………………….. Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam WATOTO Mapacha ambao mama yao amepata changamoto ya maradhi ya moyo muda mfupi tangu alipojifungua wakazi wa Kongowe Kibaha mkoani…

Read More

Morocco kuwapa wanawake haki zaidi

  RABAT. Morocco inalenga kuwapa wanawake haki zaidi ya malezi pamoja na kupinga ndoa za wake wengi, katika mapitio ya kwanza ya kanuni za familia katika kipindi cha miaka 20, mawaziri wa haki na masuala ya Kiislamu walisema Jumanne. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea). Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, wanaharakati wa…

Read More

Mugango, Sirari kuanza kufurahia huduma za kifedha

Musoma. Benki ya CRDB imefungua matawi mawili mapya mkoani Mara, Mugango (Musoma Vijijini) na Sirari (Tarime), ikiwa ni sehemu ya jitihada za kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kaulimbiu ya ‘ulipo, tupo’. Ofisa Mkuu wa Biashara wa CRDB, Boma Raballa amesema matawi hayo yameanzishwa kutokana na mahitaji makubwa ya huduma za kifedha katika shughuli za…

Read More

Hivi ndivyo mabibi na mababu walivyopanga uzazi

Unajua kama zamani licha ya kutokuwapo kwa vidonge na njia za kisasa za upangaji uzazi, bado wazee wetu hawakuwa nyuma katika kupanga uzazi? Nini walichokuwa wakifanya?Jibu unalo hapa. Ni hivi kilichokuwa kikifanyika ni baba kulazimika kukaa mbali na mkewe kwa miaka mitatu kutoka siku mama alipojifungua. Ofisa Elimu wa Kijiji cha Makumbusho, Wilhelmina Joseph, anasema…

Read More