Mugango, Sirari kuanza kufurahi huduma kifedha

Musoma. Benki ya CRDB imefungua matawi mawili mapya mkoani Mara, Mugango (Musoma Vijijini) na Sirari (Tarime), ikiwa ni sehemu ya jitihada za kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kaulimbiu ya ‘ulipo, tupo’. Ofisa Mkuu wa Biashara wa CRDB, Boma Raballa amesema matawi hayo yameanzishwa kutokana na mahitaji makubwa ya huduma za kifedha katika shughuli za…

Read More

Mabibi, mababu walivyojua majira kabla ya saa

Ulishajiuliza kabla ya ujio wa saa, mababu zetu walijuaje nyakati? James Mfikwa, mhifadhi kijiji cha Makumbusho anaeleza kwa undani njia walizotumia wahenga  katika kujua muda na kufanya shughuli zao. Kikubwa anasema walitumia jua na kivuli kufahamu majira ya asubuhi, mchana, alasiri na jioni. “Kwa mfano, mtu akisimama sehemu ambapo hakuna msongamano wa miti au jengo,…

Read More

Hali tete Msumbiji, Tanzania yakaa mguu sawa

Dar es Salaam. Ghasia zinazoendelea nchi jirani ya Msumbiji zimesambaa maeneo tofauti nchini humo wakati vyombo vya ulinzi na usalama vya Tanzania vikiimarisha ulinzi katika mipaka ya kusini huku Serikali ikiwatoa hofu wananchi waishio Mtwara. Tanzania na Msumbiji zimepakana, kwa maana ya Mkoa wa Mtwara, umepakana na Mkoa wa Cabo Delgado uliopo kaskazini mwa Msumbiji…

Read More

Prisons yailiza Pamba Jiji Sokoine

Baada ya kupoteza mechi iliyopita kwa mabao 4-0 dhidi ya Yanga, Tanzania Prisons imemalizia hasira zao kwa Pamba Jiji kufuatia ushindi wa bao 1-0. Ushindi huo unakuwa wa kwanza katika mechi mbili kwa kocha Shaban Mtupa aliyekabidhiwa majukumu kwa muda wakati aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mbwana Makata akisubiri hatma yake na mabosi. Katika…

Read More

Waethiopia wataadhimisha Krismasi yao Januari 7

Wakati Wakristo wakisherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo kama mwokozi wa dunia Desemba 25, maeneo mengine kumekuwa na matukio tofauti huku baadhi ya Wakristo wakisubiri Krismasi yao Januari 7, 2025. Akihubiri katika ibada ya Krismas, Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ametumia baraka yake ya ‘urbi et orbi’ (kwa jiji na kwa dunia) ya mchana…

Read More

Tisa wafariki dunia ajali ya basi, Noah Rombo

Rombo. Watu tisa wamefariki dunia katika Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro baada ya gari dogo aina ya Toyota Noah kugongana uso kwa uso na basi la abiria Kampuni ya Ngasere. Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Raymond Mwangwala amethibitisha kutokea ajali hiyo leo Alhamisi Desemba 26, 2024 ambapo amesema miili hiyo imepelekwa Hospitali ya Karume, wilayani…

Read More

Medo amrudisha Amza Kagera Sugar

KLABU ya Kagera Sugar iko katika hatua za mwisho za kumrejesha aliyekuwa mshambuliaji wa kikosi hicho raia wa Cameroon, Moubarack Amza kutoka Namungo, ikiwa ni pendekezo la kocha wa timu hiyo Mmarekani, Melis Medo kwa viongozi wa klabu. Nyota huyo anarejea ndani ya kikosi hicho kwa mara ya pili baada ya awali kujiunga nayo Januari…

Read More

Watano wahofiwa kufariki ajali ya basi, Noah Rombo

Rombo. Watu zaidi ya watano wanahofiwa kufariki dunia katika Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro baada ya basi la abiria Kampuni ya Ngassero kugongana na basi dogo la abiria aina ya Toyota Noah eneo la Tarakea wilayani humo. Akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu leo Desemba 26, 2024 Mkuu wa Wilaya hiyo, Raymond Mwangwala ambaye…

Read More