Mabehewa 264 ya mizigo yatakayotumika katika reli ya kiwango cha kimataifa – SGR yamewasili Bandari ya Dar

Shirika la Reli Tanzania – TRC linautaarifu umma kuwa mabehewa 264 ya mizigo yatakayotumika katika reli ya kiwango cha kimataifa – SGR yamewasili Bandari ya Dar es Salaam kutoka nchini China Disemba 24, 2024. Zoezi la ushushaji kutoka kwenye Meli litakapokamilika litafuatia zoezi la majaribio ambalo litajikita katika kutembeza mabehewa hayo kwenye Reli yakiwa tupu…

Read More

11 wafariki ajali ya Coaster, lori Handeni

Handeni. Ikiwa ni siku chache tangu wafariki dunia watu wanane, kutokana na ajali ya gari wilayani Handeni mkoani Tanga, jana usiku Desemba 25, 2024 wengine 11 wamefariki huku 13 wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha Coaster na Fuso wilayani humo. Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Albert Msando amethibitisha kutokea…

Read More

Utititri wa Wachina kila kona ni fursa au janga?

Takwimu zikionyesha kuwa China ndiyo mbia namba moja wa biashara na uwekezaji nchini, kumekuwa na mchanganyiko wa mawazo juu ya wingi wa raia Taifa hilo namba mbili kwa uchumi duniani. Wapo wanaoona wingi wa Wachina nchini ni fursa ya maendeleo kwa kuongeza shughuli za kiuchumi na wengine wakihofu kuibuka kwa unyonyaji mpya wa uchumi na…

Read More

Hatifungani hii ni ya zawadi za sikukuu

Msimu huu wa sikukuu unahusu zawadi, kutoa na kupokea. Ikiwa umejipatia zawadi ya fedha au unapanga kujinunulia kitu cha thamani, ni wakati mwafaka kufikiria jinsi unavyoweza kutumia zawadi hii kwa njia yenye manufaa zaidi. Mojawapo ya njia bora ni kuwekeza katika Hati Fungani ya Miundombinu ya Samia, mpango wa kipekee unaolenga kuharakisha maendeleo ya barabara…

Read More

‘Top 5’ magari yaliyonunuliwa zaidi Tanzania mwaka 2024

Wakati zikisalia siku kufunga mwaka 2024, yapo mengi ya kufahamu kuhusu ulivyokuwa mwaka, miongoni mwake ni magari yaliyobamba katika kipindi hicho, yaani ni yapi yalinunuliwa zaidi. Tanzania ina viwanda vichache vya kuunda/kuunganisha magari na sehemu kubwa ya magari yanayotumiwa nchini yameagizwa kutoka nje ya nchini, hususan Japan na Afrika Kusini na yaliyo mengi ni yaliyokwisha…

Read More

AKILI ZA KIJIWENI: Vita ya mastraika Ligi Kuu sio mchezo

MSIMU uliopita nyota wawili wanaocheza nafasi ya kiungo, Feisal Salum na Stephane Aziz Ki ndio walishindana katika kuwania ufungaji bora wa Ligi Kuu. Mshindi wa kinyang’anyiro hicho akawa ni Stephane Aziz Ki ambaye alimaliza msimu akiwa amefunga mabao 21 na Feisal Salum akamaliza katika nafasi ya pili akifumania nyavu mara 19. Hapa kijiweni kukaibuka makundi…

Read More