
Zanzibar yapiga ‘stop’ upigaji makachu Forodhani
Dar es Salaam. Mamlaka ya Mji Mkongwe Zanzibar imepiga marufuku upigaji wa makachu katika eneo la bustani ya Forodhani, baada ya kudaiwa kufanyika vitendo vinavyokiuka maadili. Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo jana Jumapili, Desemba 22, 2024 imeeleza uamuzi huo umefikiwa baada ya kuona kuna ukiukwaji wa sheria, kanuni na miongozo yaliyojitokeza kwa vijana wa makachu…