
Kigogo ofisi ya Msajili wa Hazina, bintiye wafa ajalini Same
Dar es Salaam. Ajali zinazotokea msimu wa sikukuu zimeendelea kuacha majonzi kwa Watanzania, baada ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu ofisi ya Msajili wa Hazina, Amos Nnko kufariki dunia. Nnko amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Same, mkoani Kilimanjaro, jana mchana Jumapili, Desemba 22, 2024. Katika ajali hiyo, pia…