
2024 mwaka wa kizungumkuti ajali za barabarani
Dar es Salaam. Ajali za barabarani zimeendelea kuwa chanzo cha vifo vya Watanzania, hali inayozua maswali iwapo hatua zinazochukuliwa na mamlaka mbalimbali nchini kama zinakidhi katika kukabiliana na changamoto hii. Katika ajali hizi, mwendo kasi umebainika kuwa moja ya sababu, zingine zikitajwa kuwa ni matumizi ya vilevi, miundombinu zikiwamo barabara zenye mashimo, zisizo na alama…