
Mpango tata wa kutoa chango kwa mifugo Kenya kuanza Januari – DW – 19.12.2024
Hata hivyo, mjadala kuhusu utekelezaji wa zoezi hilo umeibua hisia kali, huku baadhi ya madaktari wa mifugo na wafugaji wakipendekeza usitishwe, kutokana na wasiwasi kuhusu uingiliaji wa wanasiasa, ulioathiri imani ya wananchi kwa zoezi hilo. Waziri wa Kilimo na Mifugo nchini Kenya, Dakta Andrew Karanja, ametangaza kuwa mpango wa kuwachanja mifugo utazinduliwa kama ilivyopangwa mapema…