
Mpango wa kufuatilia mienendo ya viongozi wa umma kuanza mwakani
Musoma. Serikali imetangaza mpango wa kuanza kufuatilia mienendo na tabia za viongozi wa umma wanapokuwa nje ya ofisi. Imesema lengo ni kutaka kuhakikisha wanazingatia maadili na kufuata makatazo na viapo vyao kwa mujibu wa sheria. Ufuatiliaji huo, ambao unatarajiwa kuanza mapema mwaka ujao, unalenga kubaini kama matendo ya viongozi yanalingana na maadili yanayotarajiwa na Watanzania….