
Mbowe ataka saa 48 kuamua hatima yake Chadema
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amewaomba viongozi, wanachama na makada waliofika nyumbani kwake kuwa wampe saa 48 za kutafakari ombi lao la kumtaka kuwania nafasi hiyo. Pia, amewaeleza kuwa hataingia kwenye vita itakayokibomoa chama hicho bali ataingia kwenye vita itakayokijenga. Mbowe ameyasema hayo leo Jumatano, Desemba 18, 2024 wakati akizungumza na wanachama…