
Dereva bodaboda, bondia kortini tuhuma mauaji ya mtoto wa mfanyabiashara Dodoma
Dodoma. Dereva wa bodaboda, Kelvin Joshua (27) na Tumaini Msangi (28) ambaye ni bondia, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya kukusudia ya mtoto Greyson Kanyenye (6). Washtakiwa hao wakazi wa Ipagala, Jijini Dodoma, wamefikishwa mahakamani hapo leo Jumatatu, Desemba 30, 2024 mbele ya Hakimu Mkazi, Denis Mpelembwa. Akiwasomea…