maandamano yarejea tena kudai uwajibikaji – DW – 16.07.2024
Hali ni ya wasiwasi katikati ya jiji la Nairobi ambako maduka yamefungwa na idadi ya watu wanaotembea sio ya kawaida. Polisi wanapiga doria na baadhi ya barabara zimefungwa. Polisi wamefyatua makopo ya gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya waliokuwa wanakusanyika. Moshi ulihanikiza na baadhi wanaonekana wakiosha nyuso zao. Pikipiki kadhaa zimetelekezwa wakati wa mshike mshike…