Polisi wachunguzwa kuhusu miili iliyotupwa Kenya – DW – 13.07.2024
Awali polisi walisema miili kadhaa iliyokatwakatwa ya wanawake sita iliyofungwa kwenye mifuko ya plastiki ilipatikana siku ya Ijumaa ikiwa imetupwa kwenye jalala la taka katika timbo isiyotumika huko Mukuru, kusini mwa mji mkuu, Nairobi. Mamlaka ya IPOA ilisema katika taarifa baadaye kwamba mabaki ya watu wapatao tisa ilikuwa imegunduliwa, saba ya wanawake, na kuitisha uchunguzi…