Mahakama yaamuru kutaifishwa Sh185 milioni za raia wa China
Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetaifisha Sh185.787 milioni kuwa mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya raia wa China, Xie Xiaomao kukiri shtaka la kufanya biashara ya kubadilisha fedha za kigeni bila kuwa na leseni inayotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Mahakama pia imemhukumu Xiaomao (38) kulipa…