Wafanyabiashara Kariakoo wafunga Barabara ya Lumumba Dar

Dar es Salaam. Baadhi ya wafanyabiashara wanaodai majina yao kutokuwamo kwenye orodha ya watakaorejea Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam, wamegoma kuondoka katika Barabara ya Lumumba, kwenye ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM. Wamechukua uamuzi huo wa leo Alhamisi, Julai 11, 2024 baada ya kufika Viwanja vya Mnazi Mmoja kuhakikiwa upya na kueleza…

Read More

Ma-DC watatu wapata ‘mashangingi’ mapya Mara

Musoma. Wakuu wa wilaya tatu za mkoa wa Mara za Bunda, Rorya na Serengeti wamekabidhiwa magari mapya ili kuwasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao, ikiwamo usimamizi wa miradi ya maendeleo. Magari hayo matatu ni miongoni mwa ‘mashangingi’ sita ambayo Serikali inatarajia kuwapatia wakuu wa wilaya zote sita za Mkoa wa Mara katika kipindi cha mwaka…

Read More

M/RAIS AKIHANI MSIBA KWA WANAKIJIJI KASUMO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiifariji familia na waombolezaji mbalimbali kufuatia kifo cha Bi. Doleta Minya kilichotokea tarehe 09 Julai 2024. Makamu wa Rais ametoa pole hizo wakati alipoitembelea familia ya marehemu akiwa Kijiji Kasumo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma tarehe 11 Julai 2024.

Read More

Jumla ya waombaji 16,646 wamechaguliwa kujiunga kwenye vyuo 221 kwa programu ya Afya na Sayansi Shirikishi

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limesema jumla ya wombaji 16,646 wamechaguliwa kujiunga kwenye vyuo 221 vinavyotoa programu mbalimbali za Afya na Sayansi Shirikishi. Akizungumza mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Twaha Twaha MENEJA was Kitengo cha Utunuku na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Udahili, Utahini…

Read More

JKT Tanzania yatangaza vita ya ubingwa 2024/25

JKT Tanzania imesema msimu huu inapambana kuhakikisha inachukua ubingwa wa Ligi Kuu ambao unatetewa na Yanga na kushiriki michuano ya kimataifa. Akizungumza na waandishi wa habari leo Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Masau Bwire alisema kama klabu wamejipanga kubeba kila taji mbele yao ikiwemo la Ligi Kuu. Masau alisema anaamini usajili bora waliofanya…

Read More