Wachezaji wa Uruguay wazozana na mashabiki baada ya kupoteza kwenye nusu fainali ya Copa America

Nyota wa Liverpool, Darwin Nunez na wachezaji wengine wa Uruguay walihusika katika mzozo na mashabiki wa Colombia ambao ulizuka baada ya kushindwa 1-0 katika nusu fainali ya Copa America Jumatano. Mshambulizi wa Uruguay, Nunez alifyatua ngumi nyingi kwa mashabiki wa Colombia baada ya kuruka ndani ya watazamaji walioketi kwenye Uwanja wa Charlotte’s Bank of America…

Read More

Gor Mahia yaanza Kagame na kipigo

MABINGWA wa Kenya, Gor Mahia ‘K’Ogalo’ imeanza vibaya michuano ya Kombe la Kagame, baada ya kulambwa bao 1-0 na Red Arrows ya Zambia katika mechi ya Kundi B, uliopigwa jana usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam. Bao lililoizamisha K’Ogalo liliwekwa kimiani dakika ya 73 kupitia James Chamanga na kuwafanya mabingwa hao…

Read More

Waliokatwa Soko la Kariakoo waandamana ofisi za CCM Lumumba

Dar es Salaam. Wafanyabiashara zaidi ya 800 wanaodai majina yao hayamo kwenye orodha ya watakaorejea katika Soko la Kariakoo jijini Dar es Salaam, wamekusanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kujiorodhesha, kisha wakaandamana kwenda ofisi za CCM Lumumba kulalamika. Wafanyabiashara hao ni miongoni mwa waliohamishiwa kwenye masoko mbalimbali baada ya kuungua Soko la Kariakoo, kupisha ukarabati…

Read More

Mwabukusi auweka njiapanga uchaguzi TLS, kesi yafunguliwa

Mwanza. Sakata la uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) limeendelea kuchukua sura mpya baada ya mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Ziwa, Steven Kitale kufungua shauri la mapitio ya kimahakama dhidi ya TLS. Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi, leo Jumatano, Julai 10, 2024, Kitale amesema katika shauri hilo namba 16018/2024, lililofunguliwa Mahakama…

Read More

Safari ya Aziz Ki na Yanga – MWANAHARAKATI MZALENDO

Tangu Aziz Ki alipojiunga na klabu ya Yanga msimu wa 2022/2023, mashabiki wa soka hasa hasa wa Yanga wamekuwa na kitu cha ziada cha kufurahia kila mechi. Kijana huyu mwenye kipaji cha kipekee amekuwa kielelezo cha ustadi, umahiri, na uhodari kwenye timu ya Yanga SC. Kila mara anapokanyaga uwanja, ni kama nyota inayong’ara usiku wa…

Read More

Ajali ya basi Manyoni yajeruhi 28

Singida. Watu 28 wamejeruhiwa katika ajali baada ya basi la kampuni ya Zube Trans lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza kupinduka. Ajali hiyo imetokea leo Julai 11, 2024 asubuhi katika eneo la Njirii, Itigi mkoani Singida. Mganga Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Dk Furaha Mwakafwila amesema wamepokea majeruhi 28, kati yao wanawake ni 15…

Read More