Dawa 127 za asili zasajiliwa, ipo ya Kisukari
Dar es Salaam. Wakati mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) akiwa amekamilisha utafiti wake na kutengeneza dawa ya kisukari inayotumia mitishamba, Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala limesema hadi Juni 2024 dawa 127 zimesajiliwa. Mbali na kusajiliwa kwa dawa hizo, baraza limeweka wazi kuwa hakuna dawa ya figo wala Ukimwi iliyosajiliwa kwa sababu…