Modi amuhimiza Putin kutafuta amani kwa njia ya mazungumzo – DW – 09.07.2024
Waziri Mkuu Modi alitoa matamshi hayo kwenye televisheni, alipokutana na Rais Putin katika Ikulu ya Kremlin, kwenye ziara yake nchini Urusi. “Mheshimiwa, vita, mapambano, au mashambulizi ya kigaidi, kila mtu anayeamini katika ubinadamu anahisi uchungu watu wanapopoteza maisha. Na hata huko, watoto wasio na hatia wanapouawa, kuna mtu anayewaona wanakufa, moyo unauma, ni maumivu yasiyovumilika,…