Hemed: Wazanzibari badilisheni mitazamo kazi za hotelini
Unguja. Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman Abdalla, amesema licha ya kuwapo malalamiko kuwa kazi za hoteli kisiwani humo zinatolewa kwa wageni, changamoto ipo kwa wazawa kutothamini kazi hiyo, hivyo kuwataka wabadilishe mitazamo yao. Amesema kazi za hoteli na sekta ya utalii zinahitaji kujituma, hivyo wanaopata bahati kuajiriwa, wazingatie utoaji wa huduma bora….