Hofu makaburi yakigeuzwa ‘gheto’ Mbeya
Mbeya. Hofu imezuka maeneo jirani na makaburi ya Sabasaba jijini Mbeya, baada ya watu wasiojulikana kuyageuza sehemu ya kulala huku wakijifunika nguo nyeupe mithili ya sanda. Kwa mujibu wa wakazi wa maeneo hayo, si ajabu kukuta nazi zimevunjwa, vyungu na wakati mwingine watu kuogeshana hadharani katika njiapanda iliyopo karibu na makaburi hayo. Mwananchi kwa takriban…