Vijiji ndani ya Ruaha vyabakia vitano kutoka 27

Iringa/Mbarali. Tangazo la Serikali (GN) namba 175, limepunguza idadi ya vijiji vilivyokuwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kutoka 27 na hadi vitano, ambavyo mbali na kuwa ndani ya hifadhi, wananchi wanaendelea na maisha kama kawaida. Wananchi katika vijiji hivyo vitano vya Madundasi, Msanga, Luhanga, Iyala na Kilambo wanaendelea na maisha yao wakijishughulisha na…

Read More

Lugha ya Kiswahili kuuzwa nje ya nchi

Dar es Salaam. Wakati lugha ya Kiswahili ikizidi kuchanja mbuga kwa kutambulika na kutumiwa na watu wengi ulimwenguni, lugha hiyo inafanywa bidhaa ili kuwanufaisha Watanzania. Hatua hiyo inakuja ikiwa kuna watumiaji zaidi ya milioni 500 duniani kote wanaotumia lugha hiyo adhimu.  Hayo, yameelezwa leo Julai 7, 2024 na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk…

Read More

Wahamiaji wengine wanaswa mashambani Arusha

Arusha. Wakati wimbi la wahamiaji haramu likiendelea kutikisa, wengine watatu raia wa Ethiopia walioingia nchini kwa njia za panya wamekamatwa wakiwa wamejificha kwenye mashamba ya mahindi mkoani hapa. Idadi hiyo inafikisha jumla ya wahamiaji haramu waliokamatwa na Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Arusha kufikia 31 baada ya  juzi kukamatwa wengine 28. Wahamiaji hao walikamatwa usiku…

Read More

Kagawa, Lukindo haoo KenGold | Mwanaspoti

BAADA ya kumaliza sehemu ya benchi la ufundi, KenGold imeanza kusuka kikosi chake kwa ajili ya Ligi Kuu msimu ujao kwa kunasa saini ya nyota wanne akiwamo Ally Ramadhan ‘Kagawa’. Timu hiyo bado haijaanza mazoezi baada ya kukwama wiki iliyopita kwa madai ya sababu zilizo nje ya uwezo wao na inatarajia kuingia kambini wiki hii…

Read More

Mkulima asimulia wafugaji walivyomlazimisha aache ng’ombe wale mpunga

Kilosa. Mkulima wa kijiji cha Mabwegele, Hamisi Waziri aliyeshambuliwa na wafugaji akivuna mpunga shambani kwake, amesema sababu ya shambulizi hilo ni kuwazuia kuwalisha ng’ombe mpunga aliouvuna. Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumapili Julai 7,2024  baada ya kuruhusiwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambako alikuwa akitibiwa majeraha aliyoyapata kwenye shambulio hilo, amesema kuwa…

Read More

SIO ZENGWE: Kwani kuna ulazima msajili mapro wa kigeni 12?

MWAKA  huu tumeshuhudia klabu nne za Tanzania zikitakiwa kuwalipa wachezaji fedha ama kukumbana na adhabu ya kuzuiwa kusajili msimu huu baada ya wachezaji kushinda kesi zao za madai walizozipeleka Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa). Kati ya klabu hizo nne, Yanga pekee ililazimika kulipa zaidi ya Sh800 milioni baada ya wachezaji wawili iliowaacha kuwasilisha madai…

Read More

Waziri mkuu ashiriki Marathon Iringa

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa leo ameshiriki mbio za Great Ruaha Marathon zilizofanyika ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha Ambapo lengo la kufanya mbio hizo ni kukuza utalii wa kusini na kutoa hamasa kwa jamii katika kuhifadhi mazingira Akitoa hotuba kwa washiriki wa Mbio za Great Ruaha Marathon katika…

Read More

CCM yabariki vigogo Dawasa kuwekwa kando

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeubariki uamuzi wa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso wa kuwasimamisha kazi vigogo wawili wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa). Kimesema Waziri Aweso asingechukua uamuzi huo, chama hicho kingechonganishwa na wananchi kuhusu hali ya upatikanaji wa maji katika maeneo mbalimbali ya Mkoa…

Read More