AKILI ZA KIJIWENI: Mamelodi wameonyesha ukubwa kwa Mokwena
HAIKUONEKANA kama maisha yangeenda kasi kwa kocha wa mpira Rhulani Mokwena baada ya mafanikio aliyoipa Mamelodi Sundowns. Miezi michache iliyopita aliongeza mkataba wa kuitumikia timu hiyo kwa miaka minne zaidi kwa kile ambacho kilitafsiriwa na wengi kwamba kuna imani ya uongozi kwa kocha huyo. Mataji matatu ambayo aliiongoza Mamelodi Sundowns kunyakua msimu uliomalizika yalionekana yangekuwa…