Bwire mtendaji mpya Dawasa – Millard Ayo

Mhandisi Mkama Bwire ameteuliwa kushika nafasi ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar Es Salaam (DAWASA) katika kikao maalum cha Waziri wa Maji na Bodi ya Wakurugenzi DAWASA kilichofanyika leo tarehe 03 Julai, 2024 ofisi za DAWASA Dar Es Salaam. Mhandisi Bwire ni Mtumishi wa Wizara ya Maji…

Read More

Mahakama yapokea vielelezo vinne kesi mauaji ya Masumbuko

Geita. Mahakama Kuu Masijala ndogo ya Geita, imepokea vielelezo vinne vilivyotolewa na upande wa Jamhuri katika kesi ya mauaji inayomkabili Zephania Ndalawa anayeshtakiwa kwa kosa la kumuua Thomas Masumbuko. Katika kesi hiyo iliyoko chini ya Jaji Graffin Mwakapeje vielelezo vilivyopokelewa mahakamani hapo ni pamoja na hati ya dharura ya upekuzi, shoka lililotumika kumjeruhi mtu lililotolewa…

Read More

FANYENI KAZI USIKU NA MCHANA JENGO LA TAMISEMI LIKAMILIKE – MHA. MATIVILA 

OR-TAMISEMI Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Miundombinu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhandisi Rogatius Mativila amemuelekeza mkandarasi anayejenga Jengo la Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mtumba kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha kwa haraka. Mhandisi Mativila ameyasema hayo wakati wa ziara yake katika Jengo hilo ambalo linajengwa kwenye Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma leo…

Read More

Mvutano wa kisheria, tuhuma kuchoma picha ya Rais

Dar/Mbeya. Siku nne tangu Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limkamate Shadrack Chaula (24), kijana anayetuhumiwa kuchoma moto picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, suala hilo limeibua mvutano wa kisheria, ikielezwa hakuna sheria iliyovunjwa. Akizungumza na Mwananchi leo Julai 3, 2024 kuhusu kosa la kijana huyo na lini atafikishwa mahakamani, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,…

Read More

Serikali yatoa ajira kwa vijana 150 kiwanda cha glovu Idofi

Makambako. Uzalishaji wa mipira ya mikononi (glovu) katika Kiwanda cha Idofi cha Bohari Kuu ya Dawa (MSD) kilichopo Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe, umeiwezesha Serikali kutoa ajira kwa vijana 150, huku ikiokoa Sh20 bilioni kwa mwaka zilizokuwa zikinunua kifaa tiba hicho nje ya nchi. Hayo yamebainishwa leo Jumatano Julai 3, 2024 na Kaimu…

Read More

Huyu hapa mrithi wa Chama Msimbazi

KLABU ya Simba imefikia makubaliano ya kumsajili aliyekuwa kiungo mshambuliaji wa Stella Adjame ya Ivory Coast, Jean Charles Ohoua kwa kandarasi ya miaka miwili. Nyota huyo raia wa Ivory Coast ametambulishwa ndani ya kikosi hicho ukiwa ni muda mfupi tu tangu aliyekuwa mchezaji wa timu hiyo, Mzambia Clatous Chama kujiunga na Yanga baada ya mkataba…

Read More