Wananchi wahofia kulipuka volcano Kigoma

Kigoma. Mwenyekiti wa Kijiji cha Pamila, Wilaya ya Kigoma, Obedi Tuwazaniwe ameeleza namna tope linalozaniwa kuwa volcano lilivyozua taharuki kwa wakazi wa kijiji hicho, huku  mtaalamu wa jiolojia mkoa akiwatoa hofu wananchi. Tuwazaniwe amezungumza jana Julai 2, 2024 mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo ilikwenda kujionea hali halisi kwenye eneo hilo….

Read More

Ujumbe wa Rais wa Msumbuji akiwaaga Watanzania

Dar es Salaam. Zikiwa zimebaki siku 98 kabla ya Msumbiji kufanya uchaguzi wake mkuu, Rais wa Taifa hilo, Filipe Nyusi amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika safari yake ya utawala wa miaka 10. Rais Nyusi amesema hayo leo Jumatano, Julai 3, 2024, katika sehemu ya hotuba yake ya ufunguzi wa Maonyesho ya 48 ya…

Read More

Kaseba, Mandonga kuzipiga Mikoani | Mwanaspoti

BINGWA wa zamani wa Kick Boxing wa Dunia, aliwahi pia kutamba kwenye Ngumi za Kulipwa nchini, Japhet Kaseba sambamba na Karim Mandonga ni miongoni mwa mabondi watakaozipiga katika mapambano maalumu ya hisani ya kusaidia jamii kupata Bima ya Afya. Mabondia hao na wengine watapambana mapambano hayo ya ngumi yatakayofanyika mwishoni mwa mwezi huu yakiandaliwa na…

Read More

Kampuni 11 za Tanzania zaanza kunufaika biashara AfCFTA

Dar es Salaam. Kampuni 11 za Tanzania zimeanza kunufaika na ufanyaji wa biashara katika Eneo Huru la Biashara la Bara la Afrika (AfCFTA). Kampuni hizo zimeanza kutumia fursa kwa kusafirisha bidhaa za kahawa, katani, viungo, karanga na tumbaku kwenda nchi mbalimbali Afrika ikiwemo Nigeria, Ghana, Algeria na Morocco. Hayo, yamebainishwa na Rais Samia Suluhu Hassan…

Read More

Lugalo Open yateka wapiga fimbo 150 Dar

VUMBI na nyasi kutimka katika viwanja vya gofu vya Lugalo, ambavyo vitakuwa ni shuhuda wa miamba  zaidi ya 150 watakaokuwa kuwania tuzo mbalimbali za mashindano ya wazi ya gofu yanayoanza kesho. Yakija kwa jina rasmi la Lugalo Open, ni mashindano ya siku tatu yatakayowashirikisha wacheza gofu ya kulipwa (mapro) na wale wa ridhaa, kwa mujibu…

Read More

Biteko: Bora uitwe mshamba, lakini usimamie maadili

Dar es Salaam. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk Doto Biteko amesema kuna umuhimu mkubwa kwa jamii, wakiwamo vijana, wazazi, wanafunzi na Serikali kwa ujumla, kusimamia maadili ya Kitanzania. Amesema ni bora mtu uitwe mshamba, lakini asimamie misingi na tabia zote njema zinazotambulika katika jamii na kuachana na maadili yasiyofaa. Biteko ameyasema hayo…

Read More

Mufti azindua kitabu chake – Mtanzania

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dk. Abubakar Zubeir, amezindua kitabu chake kiitwacho ‘Mmomonyoko wa Maadili Nani Alaumiwe?’, ambapo amesema kilichomsukuma kufanya hivyo ni hali ya kumomonyoka kwa maadili iliyopo kwa sasa nchini. Kitabu hicho chenye sura saba kimezinduliwa leo Julai 3,2024, BAKWATA Makao Makuu, jijini Dar es Salaam…

Read More