Takukuru yataja athari za rushwa kwenye uchaguzi
Dar es Salaam. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imesema rushwa ni chanzo cha kupatikana viongozi wasio na maadili, wasiozingatia misingi ya haki, usawa, uwazi, uwajibikaji na uzalendo. Taasisi hiyo pia imesema rushwa inadhoofisha utawala bora na demokrasia na baadhi ya wananchi wenye sifa za uongozi bora hushindwa ama kugombea, kutoteuliwa au kuchaguliwa…