TRA, ZRA zikiongeza ufanisi, wachumi watia neno kuhusu mikopo

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza ufanisi katika makusanyo ya mapato yaliyofikia asilimia 97.67 katika mwaka wa fedha 2023/24, yakiwa yameongezeka kwa asilimia 14.5 ikilinganishwa na ya mwaka 2022/2023 Kufuatia ongezeko hilo, wataalamu wa uchumi wamesema ni vyema sasa nchi ikaanza kufadhili miradi yenyewe na kupunguza utegemezi wa mikopo kutoka nje. TRA…

Read More

Kesi madai ya ukahaba, Mahakama yaikomalia Serikali

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Sokoine Drive, jijini Dar es Salaam imezidi kuikaba kooni Serikali kuhusiana na uthibitisho wa ugonjwa wa shahidi wake aliyeshindwa kutoa ushahidi katika kesi ya ukahaba wiki iliyopita kwa maelezo anaumwa. Ni baada ya kuionya Serikali na kuitaka iheshimu amri na mamlaka ya mahakama. Mbali na onyo hilo, ingawa…

Read More

Vikwazo ukuaji magari, pikipiki za umeme Tanzania

Dar es Salaam. Uhaba wa wataalamu, kodi kubwa na changamoto za kisera ni miongoni mwa vikwazo vilivyotajwa kusababisha idadi ndogo ya vyombo vya moto vinavyotumia nishati ya umeme katika uendeshaji wake nchini. Kwa mujibu wa Ripoti ya E Mobility Alliance iliyotolewa Machi 2023, Tanzania ina vyombo vya moto vinavyotumia umeme 5,000 idadi ambayo ni ndogo…

Read More

Tanzania, Msumbiji kuanzisha kituo kimoja cha forodha

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema yeye pamoja na Rais wa Msumbiji, Philip Nyusi wamekubaliana kuanzisha sasa kituo kimoja cha forodha Mtambaswala kitakachohamasisha biashara. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea). Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumanne wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Rais wa Msumbiji, Philip Nyusi Ikulu jijini Dar es…

Read More

Mtandao wa X ulivyomtoa Matarra gerezani

Dar es Salaam. “Nilipokuwa si kuzuri hata kidogo, nawashukuru wanamtandao wa X.” Haya ni maneno ya Japhet Matarra, kijana aliyechiwa huru baada ya kufungwa gerezani kwa makosa ya mtandao. Kijana huyo aliyetiwa hatiani kwa kuhoji utajiri wa marais wa Tanzania kupitia mitandao ya kijamii, ameachiwa baada ya marafiki na wanaharakati kuchangisha fedha kupitia mtandao wa…

Read More

Azam waipa Simba bei ya Fei Toto

SIMBA na Mamelodi Sundowns zimeulizia uwezekano wa kumsainisha mkataba staa wa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ lakini zikaambiwa hauzwi. Fei Toto ambaye alitua Azam FC akitokea Yanga, alisaini mkataba wa miaka mitatu na tayari ameutumikia kwa msimu mmoja akiisaidia timu hiyo kumaliza katika nafasi ya pili na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika Ligi…

Read More

EST waja na mwarobaini kuwadhibiti wachumi ‘makanjanja’

Dar es Salaam. Jumuiya ya Wachumi Tanzania (EST), imesema umefika wakati wachumi nchini wanapohitimu elimu ya juu, wanapaswa kufanya mtihani wa kupima ubobezi wao katika taaluma hiyo. Hayo yameelezwa leo Jumanne Julai 2, 2024 na mratibu wa jumuiya hiyo, Geofrey Mwambe, alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la wanajumuiya wa uchumi linalotarajiwa kufanyika Julai…

Read More