Mahamakama yamwachia huru aliyedaiwa kumuua mwanawe
Geita. Mahakama Kuu kanda ya Geita imemuachia huru Stephano Mlenda (31) Mkazi wa Chigunga Wilaya ya Geita, aliyekuwa akishtakiwa kwa kosa la kumuua mtoto wake wa miaka tisa kwa kutokusudia. Baba huyo anadaiwa kumchapa kwa fimbo mwanawe huyo baada ya kubaini ameiba Sh700 na kwenda kununua soda. Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatatu Julai Mosi, 2024…