Udanganyifu wa ‘mashamba boi’ wapata muarobaini
Dar es Salaam. Wabunifu wamekuja na kifaa cha kukomesha udanganyifu wa wasimamizi wa mashamba ya samaki kwa kubuni kifaa cha kulishia samaki kitakachotoa taarifa kwa mmiliki ya muda na kiasi cha chakula walichopewa. Ili kupatikana samaki kwa wingi ni lazima kuwe na kazi ya kupanda, kukuza na kuwatunza katika bwawa au uzio uliotengenezwa kwa vyuma,…