Magamba ya samaki kaa kuzalisha nyuzi, nguo, ‘tishu’

Dar es Salaam. Katika kusaidia mapambano ya uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na utupaji taka holela, mwanafunzi wa shahada ya uzamili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), amebuni namna magamba ya samaki aina ya kaa yanavyozalisha nyuzi na nguo. Magamba hayo ya kaa ambayo kwa sasa huishia madampo katika maeneo mbalimbali, yanapochanganywa na mwani,…

Read More

Mbowe: Kuwa Chadema sio suala jepesi

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe amesema mtu kuwa chama cha upinzani inahitaji ujasiri. Mbowe ametumia kurasa zake za kijamii kuelezea maisha ya wanasiasa ndani ya upinzani na wale walioko chama tawala. Ujumbe huo unasomeka: “Kuwa chama cha upinzani hasa Chadema sio suala jepesi, linahitaji ujasiri wa…

Read More

BIL 1.9 ZIMETUMIKA MATENGENEZO BARABARA ZILIZOATHIRIWA NA EL-NINO MKOANI SHINYANGA-ENG JOEL

Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt samia Suluhu Hassan imetoa fedha shilingi Bilioni 1.9 kwa ajili ya kushughulikia barabara zilizoathiriwa na Mafuriko/mvua za Elnino kwa Mkoa wa Shinyanga. Fedha hizo zimetumika kuhakikisha kuwa miundombinu yote ya barabara iliyoathirika na wananchi kushindwa kutoka eneo moja kwenda jingine inapitika kwa haraka…

Read More

Tyla aanza kwa kishindo katika Tuzo za BET 2024

Mwanamuziki kutokea Afrika ya Kusini mwnadada Tyla aliufanya umati wa watu kucheza  wimbo wimbo wake mpya zaidi katika Tuzo za BET 2024 ambao umetamba kwa muda sasa. Jumapili, Juni 30, kwa mara ya kwanza katika usiku wa kitamaduni mkubwa zaidi katika Ukumbi wa Tamthilia ya Peacock huko Los Angeles alitoa burudani isiyosahaulika huku Gunna na…

Read More

Mpya wafanyabiashara Musoma wafunga mageti ya soko

Musoma. Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Manispaa ya Musoma mkoani Mara, wamefunga milango ya kuingia sokoni hapo, wakishinikiza kuondolewa kwa wafanyabiashara ndogondogo ‘machinga’ wanaofanya shughuli zao kuzunguka soko hilo. Wafanyabiashara hao wamegoma kuingia sokoni wakidai mazingira ya kufanya biashara sio rafiki. Wakizungumza wakiwa nje ya soko hilo leo, Jumatatu, Julai mosi, 2024, wamesema hawatafungua milango…

Read More

TANROADS yampa tano rais Samia kutoa Bil 101.2 kuanza ujenzi barabara ya Kahama-Bulyanhulu JCT – Kakola

Baada ya tarehe 16 Machi 2024 Serikali kusaini Mkataba wa ujenzi wa barabara ya Kahama-Bulyanhulu Jct – Kakola yenye urefu wa Kilomita 73 kwa kiwango cha lami, tayari Kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation imeanza utekelezaji wake. Pamoja na Barabara hiyo kufungua fursa za kiuchumi za madini, kilimo, misitu na utalii katika mikoa ya…

Read More

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI: BENKI YA NCBA YAZINDUA SHINDANO LA NCBA GOLF SERIES 2024 KATIKA KLABU YA ARUSHA GYMKHANA

Shindano la NCBA Golf Series 2024 ilimezinduliwa rasmi leo katika Klabu ya Arusha Gymkhana, na kuleta pamoja jamii ya wapenzi wa gofu na dhamira ya kujenga utamaduni wa michezo huo.  Benki ya NCBA, taasisi ya kifedha inayoongoza nchini Tanzania, inajivunia kuandaa tukio hili, ikionyesha dhamira yake ya kushirikiana na jamii na kukuza utamaduni mzuri wa…

Read More

TRC kuongeza safari treni ya SGR Dar -Morogoro

Dar es Salaam. Shirika la Reli Tanzania limetangaza ongezeko la safari za treni ya kisasa (SGR) zitakazohusisha kuanza kwa treni mpya ya mwendo kasi (Express train) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro bila kusimama vituo vya kati. Ratiba iliyotolewa inaonyesha kutakuwa safari nane kwa siku na treni hizo zitakuwa zinapishana kwa takribani dakika 20 kati…

Read More