Kinachomsibu Sativa akipatiwa matibabu Aga Khan

Dar es Salaam. Ripoti ya awali ya vipimo kutoka kwa madaktari wa Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam, imeonyesha Edgar Mwakabela maarufu kama Sativa, amepata mpasuko wa taya zilizosagika, huku baadhi ya mifupa ikionekana na mipasuko midogo. Sativa anayejishughulisha na biashara ya miamala ya fedha na michezo ya kubahatisha, alichukuliwa vipimo usiku wa…

Read More

Vikoba vyatajwa malezi mabovu kwa watoto

Katavi. Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Mariam Sagini amesema wanawake wengi wamesahau jukumu lao kubwa la kuzaa na kulea familia  kwa sababu ya vikundi vya kijamii vikiwamo vya vikoba. Amesema hali hiyo inachangia kuporomoka kwa maadili ya watoto na vijana nchini. Akizungumza katika Kikao cha Baraza la UWT Mkoa…

Read More

Serikali kudhibiti taarifa holela utaalamu wa kilimo

Arusha. Katika kukabiliana na taarifa zinazokinzana na zinazowachanganya wakulima kuhusu huduma za ugani, Serikali imeanza matumizi ya mfumo wa usajili na habari kidijitali, ili kuwawezesha wakulima kupata taarifa sahihi na za kuaminika. Mifumo hiyo iliyotolewa na Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) inalenga kuendeleza mabadiliko ya kilimo kidijitali kote nchini, ikishughulikia changamoto kadhaa  ambazo zimekuwa…

Read More

Mfugaji wa Kimasai adaiwa kuua mtu kwa rungu Kilosa

Morogoro. Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma Nzigula, mkazi wa Peapea, Kata ya Ludewa, Wilaya ya Kilosa mkoani hapa, amefariki dunia baada ya kudaiwa kupigwa rungu kisogoni na mfugaji wa jamii ya Kimasai. Inadaiwa kuwa Mmasai huyo alimpiga Nzigula baada ya kudai kummulika kwa tochi usiku wakati akitoka kwenye majukumu yake. Akizungumza na Mwananchi…

Read More

OPAH Kwake ni soka na biashara

MIONGONI mwa wachezaji wanaolijua lango vizuri kwa upande wa soka la wanawake, Opah Clement yupo kwenye listi hiyo. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba Queens kwa sasa anaichezea klabu ya Besiktas inayoshiriki Ligi Kuu ya wanawake nchini Uturuki na ndio nahodha wa timu ya taifa ya wanawake, Twiga Stars. Hadi anaondoka nchini kujiunga na klabu…

Read More

Nimesikitishwa na uamuzi wa Msigwa

MJUMBE wa Kamati Kuu Chadema, Godbless Lema ameeleza kushtushwa na kusikitishwa na uamuzi wa aliyekuwa kada mwenzake wa cha hicho, Mchungaji Peter Msigwa kuhamia Chama Cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea). Lema ambaye pia alikuwa Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini na Mwenyekiti wa Chadema kanda ya kaskazini, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa…

Read More

Mpina kuwaburuza kortini Spika Tulia, Waziri Bashe

Dar es Salaam. Baada ya ukimya wa siku sita tangu alipoadhibiwa kutohudhuria vikao 15 vya Bunge, Mbunge wa Kisesa (CCM), Luhaga Mpina ametangaza mpango wa kuwaburuza mahakamani Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson. Pamoja na Dk Tulia, mbunge huyo amesema hatua kama hizo atazichukua dhidi ya Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, Bodi ya Sukari Tanzania…

Read More

Wabongo, Wakenya wakabana magari | Mwanaspoti

ITAKUWA ni mchuano mkali kati ya madereva wa Tanzania na Kenya katika mwezi huu wakati harakati za kuwaleta nchini washiriki kutoka Mombasa zikifikia hatua ya kuridhisha. Kwa mujibu wa waandaji kutoka Klabu ya Mount Usambara, kuna mchakato wa kuwaleta Tanga madereva bingwa kutoka Mombasa nchini Kenya na kwa mujibu wa mwenyekiti wa klabu hiyo, Hussein…

Read More

Mchungaji Msigwa ajiunga CCM | Mwananchi

Dar es Salaam. Aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema kanda ya Nyasa, Mchungaji Peter Msigwa amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM) na kutambulishwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC). Mchungaji Msigwa aliyewahi kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema, ametambulishwa leo Jumapili Juni 30, 2024 katika kikao hicho kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam,…

Read More