Waathirika wa mafuriko Bukoba wapewa msaada
Bukoba. Kaya 49 zenye watu 147 zilizoathirika na mafuriko katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, wamekumbukwa na Serikali kwa kupatiwa msaada wa vifaa na chakula. Kaya hizo ziliathiriwa na mvua iliyonyesha Mei 10, 2024 na kuleta maafa katika Halmashauri ya manispaa ya Bukoba na kusababisha binti mmoja aliyetambulika kwa jina la Leah (19) kupoteza maisha….