Kenya yafanya tathimini ya hali baada ya Maandamano – DW – 26.06.2024
Duru zinaeleza kwamba maiti zisizopungua 7 zilifikishwa kwenye chumba cha City jijini Nairobi.Kwa mujibu wa maafisa wa chumba hicho cha hifadhi, maiti hizo zilikuwa na majeraha ya risasi na moja ilionesha dalili za kukabwa koo. Kulingana na taratibu,maiti zinazopatikana kwenye mazingira ya vurugu na maandamano sharti zifikishwe kwenye chumba cha maiti cha serikali ili kutambuliwa…