Mgodi wa Barrick waamriwa kuifidia familia Sh150 milioni
Dar es Salaam. Mahakama ya Rufani imemuamuru meneja mkuu wa kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick Gold Mine Ltd (ABG), kuilipa fidia ya Sh150 milioni familia ya Chacha Kiguha, mkazi wa Kijiji cha Nyamwaga, wilayani Tarime, kwa madhara iliyoyapata kutokana na shughuli za mgodi. Awali, Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza iliamuru maneja huyo kuilipa…