SMZ kutobinafsisha sekta ya elimu, ZSTC

Unguja. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema haina mpango wa kubinafsisha sekta ya elimu na Shirika la Biashara la Taifa (ZSTC) kutokana na umuhimu wake na unyeti kwa masilahi ya Taifa. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi, Hamza Hassan Juma ametoa kauli hiyo Juni 25,…

Read More

RC Batilda aagiza Halmashauri Lushoto kulipa madeni

Lushoto. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Balozi Batilda Burian ameiagiza Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto kulipa deni la zaidi ya Sh700 milioni, linalodaiwa na wafanyakazi, makandarasi na watoa huduma wengine. Amesema deni hilo linaonyeshwa kwenye vitabu vya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG). Hayo amesema leo Jumanne Juni 25, 2024  wilayani Lushoto…

Read More

Rais Ruto aibua mpya maandamano ya Gen Z

Nairobi. Rais wa Kenya, William Ruto amesema maandamano ya amani ya Generation Z yaliingiliwa na wahalifu, akisisitiza Serikali itazingatia mamlaka yake ya kikatiba ya kulinda Taifa kutokana na vitendo hivyo. Amesema tukio la vurugu katika maandamano ya leo Juni 25, 2024 linatoa somo la namna ya kukabiliana na vitisho vya usalama wa Taifa. “Ninawahakikishia Wakenya…

Read More

Wanafunzi 100 wanolewa programu ya uongozi

Dar es Salaam. Wanafunzi 100 kutoka shule za sekondari nchini, wameanza kunolewa kupitia programu ya uongozi kwa vijana (Beginit), iliyotajwa kuwa chachu ya mabadiliko katika uongozi wa kijamii hapo mbeleni. Wadau wa maendeleo wanaoendesha mradi huo, wamebainisha kuwa wataendelea kushirikiana na Serikali kutoa mafunzo ya uongozi kwa vijana lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa kutambua…

Read More

NEMC: Lipeni ada ya tathmini ya mazingira kwa wakati

Dar es Salaam. Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limewataka watathmini mazingira na wawekezaji kulipa Ada za Tathmini ya  Mazingira (EIA) katika wakati uliopangwa ili kutekeleza miradi yao kwa kuzingatia sheria za mazingira. NEMC imesema muda unaotakiwa kulipwa ada na tozo hiyo kisheria ni kuanzia Julai mosi hadi Desemba 31 kila…

Read More