MRADI WA SLR WATENGA BILIONI 1.091 KUTEKELEZA SHUGHULI ZA MIRADI YA KIJAMII NA KIUCHUMI KWA WANANCHI

Maafisa Waandamizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wanaosimamia Mradi wa Urejeshwaji Endelevu wa Mazingira na Hifadhi ya Bioanuai (SLR) Bw. Julius Enock na Bi. Risper Koyi wakifuatilia uwasilishaji wa taarifa mbalimbali kuhusu Mradi huo leo Jumanne (Juni 25, 2024) wakati wa kikao kazi hicho cha Siku tatu kinachoendelea Jijini Mbeya. Baadhi ya washiriki wa…

Read More

Wanawake msisahau majukumu yenu ya kutunza familia.

Mkuu wa mkoa wa Tanga Dkt Batlida Buriani amewataka wanawake mkoani hapa licha ya kushirikisha kwenye shughuli za kujitafutia kipato wahakikishe hasahau jukumu la malezi kwa watoto wao. Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo Kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia Kwa watoto katika wilaya mbalimbali za mkoani huu jambo ambalo lina haribu ustawi wao wa…

Read More

Wafanyabiashara Mwanza waanika sababu za kufunga maduka yao

Mwanza. Wakati wafanyabiashara jijini Mwanza wakitangaza mgomo na kufunga maduka yao, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Mwanza, Patrick Masagati ametaja sababu za mgomo huo. Akizungumza na Mwananchi Digital leo Jumanne Juni 25, 2024, Masagati ametaja sababu hizo kuwa ni kupinga sheria za kodi (bila kuzitaja) zinazochangia unyonyaji na kuwarudisha nyuma wafanyabiashara. “Kitu ambacho…

Read More

DKT. Biteko akutana na wawekezaji wa Modern industrial park

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na wawekezaji wa Modern Industrial Park wanaomiliki kongani ya viwanda eneo la Kibaha, Mkoani Pwani. Mazungumzo hayo yamefanyika Juni 24 katika ofisi za Naibu Waziri Mkuu Bungeni, jijini Dodoma. Aidha, Dkt. Biteko amewaeleza wawekezaji hao kuwa Serikali iko tayari kushirikiana…

Read More

Maandamano yapamba moto Kenya, wanaharakati 10 watekwa

MAELFU ya vijana wamefurika katikati mwa barabara za miji nchini Kenya kushiriki maandamano ya kupinga Muswada wa Fedha 2024 ilihali wabunge wakiendelea kuujadili bungeni. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea). Milipuko inadaiwa kusikika katikati ya jiji la Nairobi wakati polisi wakifyatua mabomu ya machozi dhidi ya vijana wanaopinga kelele wakielezea kutoridhishwa kwao na muswada huo….

Read More

Mwabukusi, wengine watano wapitishwa kugombea urais TLS

Dar es Salaam. Mwanasheria Boniface Mwabukusi (Mbeya) ni miongoni mwa mawakili sita waliopitishwa kugombea urais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 2, mwaka huu jijini Dodoma. Mbali na Mwabukusi, taarifa iliyotolewa na kamati ya uchaguzi ya TLS jana Juni 24, 2024 imewataja wagombea wengine kuwa ni Ibrahim Bendera (Ilala),…

Read More