RC Mtambi aagiza wenye ulemavu watambuliwe, wapewe mikopo
Rorya. Mkuu wa Mkoa wa Mara, Evans Mtambi amewaagiza wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo kuwatambua na kuwezesha uanzishwaji wa vikundi vya watu wenye ulemavu katika wilaya zao. Pia amewataka kusimamia usajili wa vikundi hivyo, ili viwezeshwe kiuchumi. Mtambi ametoa maagizo hayo leo Jumatatu, Juni 23, 2024, alipofunga mafunzo ya ujasiriamali…