Fedha za Mo Dewji zimeanza kazi, Kumshusha mido Mnigeria
ILIANZA kama tetesi vile, lakini taarifa zikufikie kwa sasa kwamba Mnyama amemalizana na kiungo mkabaji, Augustine Okejepha aliyekuwa akikiichezea Rivers United ya Nigeria. Mwanaspoti liliripoti hivi karibuni juu ya dili hili la Simba na Mnigeria huyo anayetajwa kuja kuchukua nafasi ya Babacar Sarr anayetarajiwa kupewa ‘thank you’ muda wowote kuanzia sasa ili kupisha majembe mengine…