Sheikh Nyange afariki dunia Makka Saudia
Unguja. Sheikh Said Nyange (48) amefariki dunia baada ya kuugua ghafla akiwa Makka nchini Saudi Arabia alipokwenda kuhiji. Akizungumza na Mwananchi Digital, leo Jumapili, Juni 23, 2024 Katibu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (Juwaza), Muhidin Zebeir Muhidin amesema kiongozi huyo amefarikia dunia usiku wa kuamkia leo huko Saudia. “Ni kweli sheikh Said Nyange amepoteza maisha…