Simba yafuata kiungo Mashujaa | Mwanaspoti
WAKATI fagio likiendelea kutembezwa Simba, mabosi wa klabu hiyo wapo bize kuingiza majembe mapya, kwani baada ya beki Lameck Lawi, tayari imemvuta kiungo mwingine fundi kutoka Mashujaa. Simba imemsajili kiungo huyo, Omary Omary ikielezwa kashapewa mkataba wa miaka miwili na kilichobaki ni kutangazwa kama ilivyokuwa kwa Lawi aliyenyakuliwa kutoka Coastal Union iliyoamua kuikataa biashara hiyo…