Rais Samia kunogesha tamasha la Utamaduni
RAIS wa Tanzania, Dk Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Utamaduni litakalofanyika mkoani Ruvuma katika viwanja vya Maji Maji kuanzia Julai 20-27 mwaka huu. Hayo yamewekwa wazi na Naibu waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’, katika uzinduzi rasmi wa tamasha hilo uliofanyika juzi jijini Dar es Salaam….