Hivi ndivyo anavyopaswa kulala mjamzito
Dar es Salaam. Mwanamke anapopata ujauzito hupitia mabadiliko mbalimbali ya mwili na afya yake. Inaelezwa mara zote mabadiliko hayo husababishwa na mtoto aliyetumboni, lakini pia, kuongezeka kwa homoni mwilini mwake. Wataalamu wanasema mabadiliko hayo huyafanya maisha ya mjamzito kubadilika kuanzia kwenye mavazi, chakula, uwezo wa kutekeleza majukumu ya kila siku sambamba na namna ya kulala….