Sababu Polisi kumkomalia Dk Nawanda
Dar/Mwanza. Wakati waandishi watatu waliokuwa wakishikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza wakiachiwa kwa dhamana, usiri umeendelea kutanda dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahaya Nawanda kama ameachiwa au anaendelea kushikiliwa. Waandishi hao, Dinna Maningo, Mwanga Wachu na Costantine Mathias wameachiwa leo Alhamisi, Juni 20, 2024 baada ya kushikiliwa kwa siku…