Mashabiki Simba waiganda ‘Thank you’ ya Jobe
Akufukuzae hakuambii toka. Ndiyo msemo unaoweza kuutumia kwa mshambuliaji wa Simba, Pa Omar Jobe, ambaye mashabiki wa klabu hiyo wameonyesha kiu kubwa ya kutamani kuona anaachwa. Simba wiki hii, imeanza kuwaaga wachezaji wake ambao hawatawahitaji msimu ujao, ikiwa tayari imeshawaaga wawili, aliyekuwa nahodha wake mshambuliaji John Bocco, Jumatatu Juni 17 na leo ikimuaga kiungo mshambuliaji…